Charles WashomaKupendekezwa & Kukubalika

Nimepanda jumbe nyingi za namna ninavyopendekezwa na kukubalika tangu nilipoanza kufanya kazi, lakini maneno ninayoyakumbuka zaidi ni ya marehemu mkuu wangu wa shule pale nilipokuwa ninamaliza masomo ya sekondari mwaka 1991: “Ninaamini kwamba Charles atakuwa na mchango mkubwa katika maisha yake ya utu uzima na kwa dunia nzima”.

Nimepokea sifa nyingi kutokana na maarifa yangu katika masuala ya usimamizi wa mahusiano, uchanganuzi wa biashara, mikakati, uongozi shirikishi, na ushauri juu ya utawala kutoka kwa wafanyabiashara wakubwa ikiwa ni pamoja na Bwana Ibrahim Kaduma, Mwenyekiti wa shirika la African Life Assurance, Margaret Dawes, Mkurugenzi Mtendaji wa Sanlam Emerging Markets (SEM), Junior Ngulube, Mtendaji Mwandamizi wa Munich Reinsurance Africa, Harpreet Duggal, Rais wa International Markets Binani Cement, Jay Dobah, Mtendaji Mwandamizi was Mphilo Yami Insurance Brokers, Aiden Eyakuze, Mkurugenzi wa Serengeti Advisors, Wilberforce Machimbidzofa, Mkurugenzi Mtendaji wa Reinsurance Solutions Group, Philip Van Schalkwyk, Mtendaji Mwandamizi, na Innocent Nousenga, Mkurugenzi Mtendaji wa Care Insurance Brokers.

Baadhi ya Maelezo na Mapendekezo kuhusu ni haya yafuatayo:

“Charles ni kiongozi mwenye dhamira na maono. Anaaminika na mara zote kichwani kwake anamtazamo mpana zaidi wa mambo. Pamoja na majukumu yake mengi na mafanikio makubwa kwenye biashara, Charles hutumia muda wake kuhudumia viwanda na jamii kwa ujumla,jambo linaloonyesha imani yake kwamba mafanikio hayaishii kwake binafsi au kwenye biashara yake, lakini kwamba ni lazima yaenee na kwa jamii kubwa pia”

Bw. Yogesh M. Manek, Mwenyekiti Mtendaji – Kampuni ya MAC

“Charles ana maarifa, ana ari ya hali ya juu, ana dhamira ya dhati katika mambo anyoyaamini na medhamiria kwa nguvu zote kufanikiwa katika kila jambo analolifanya. Ama kwa hakika Afrika na hasa biashara ya bima ina hazina thabiti ya uongozi wa Charles Washoma”

Bw. Ibrahim Kaduma, Mwenyekiti - African Life Assurance

“Charles alikuwa mtu muhimu katika kuchangia kwenye ukuaji wa Kampuni, alipichukua tangu ilipoanzishwa kama biashara ndogo kabisa mpaka kufikia hatua ya kuwa bima ya maisha kubwa ya kuliko zote Tanzania. Haya ni mafanikio makubwa zaidi katika soko la namna hii. Charles alikuwa ni kiongozi mahiri na aliyekuwa na mahusiano mazuri na wateja na wafanyakazi”

Margaret Dawes, Mkurugenzi Mtendaji, Sanlam Emerging Markets (SEM)

“Charles ana sifa zinazotakiwa kwa kiongozi.  Charles ni mwanamawasiliano mzuri. Charles ni muadilifu na kwa sababu hiyo matendo yake yanaendana na maneno yake. Ni kiongozi mwenye maono ambaye ana uwezo wa kuona mbele kwa namna bora. Aliweza kuwavutia watu wengine nawafanyakazi wake walimuheshimu sana. Charles hutatua matatizo makubwa kiubunifu na kwa mafanikio, na kufanyakazi naye mara zote kufanya naye kazi kunafurahisha na kumekuwa kwa mafanikio”

Darlington Chamburuka, mtakwimu bima, kampuni ya Old Mutual, South Africa (2010)