Charles WashomaA life with purpose...

Ninaishi katika hofu ya Mungu. Ninaipenda familia yangu na ninajali ustawi wa jamii yangu na binadamu wote. Mimi ni Mwanachama wa mpango wa kifahari wa Ushirika wa Uongozi wa Askofu Mkuu wa Tutu unaofadhiliwa na Taasisi ya Afrika ya Uongozi (AfLI) na Chuo Kikuu cha Oxford (UK). Nimeteuliwa na kusajiliwa kama mjumbe wa Jukwaa la Crans Montana Forum of New Leaders for the Future.
Mwezi Novemba 2000 nilipewa tuzo ya Utumishi Uliotukuka wa Junior Achievement Zimbabwe “kwa ajili ya Huduma Iliyojipambanua kwa Vijana na  Jamii na kwa Kujitoa na kwa Ubora katika kuwafundisha vijana maadili, ufanyaji kazi na Ufundishaji bora matokeo ya mfumo wa Mashirika Shindani kwa kupitia mpano wa Juniour Achievement”.

“Ninaamini kwamba mioyoni mwetu sote ni viongozi na tunachohitaji ni nia ya kukua katika uwezo wetu wa uongozi na kuwa aina ya viongozi kwa namna tunavyopaswa tuwe.”

Curriculum Vitae

Services Offered

Ninajiungana watu, taasisi ambazo kwa ujumla dhima na maadili yao yanaendelea na yangu. Kila siku ninaishi kwa kadri ya makusudio na maadili yangu, ili niweze kutimiza malengo yangu hatua kwa hatua na ninazishaushi jamii ninazoishi nazo.

Huduma na Majawabu

Ninatambua kuwa uongozi nunaanza na binadamu mmoja halafu unatapakaa katika ngazi zote za jamii ikiwemo familia, mahala pa kazi, jamii, mataifa na dunia nzima. Nitatoa kanuni pana na majawabu ambayo yatagusa kada zote za jamii kwa kusudi la kujenga jamii ya watu walio na hamasa, familia zilizo imara, na mahali pa kazi penye tija kwa kusudio la kupata jamii unganifu na dunia nzuri zaidi.

Bookmark and Share

Uongozi

Kiongozi katika Biashara & katika Jamii – nimejidhatiti katika uadilifu, huduma bora, kujifunza na ubunifu. Nimejikita zaidi katika maendeleo ya makampuni na watu nikikuza maendeleo ya mtu mmoja mmoja pamoja na mafanikio na faida ya mashirika. Ninafahamika kwa kuchagua mkakati sahihi wa soko, kuandaa dira na kushawishi ufikiwaji wa malengo husika; muumini imara wa ubepari wenye dhamira njema na watu.

Uzoefu wangu hai wa uongozi ni wa muda wa miaka 22, kuanzia Afrika ya Mashariki na Kusini mwa Afrika mpaka Uingereza na Kanada. Mapenzi yangu ya dhati ya mabadiliko ya jumuiya na uongozi yalianza tangu nikiwa na umri mdogo, baada ya kuhudumu kama Diwani Mtoto na Meya Mtoto wa mji wangu huko Bulawayo, Zimbabwe nikiwa na umri wa miaka 17, nikiwa Kiranja Mkuu (Kiongozi wa Wanafunzi) wa Shule ya Sekondari ya Hamilton, na pia kama Balozi Mtoto wa British Columbia, huko Kanada katika umri wa miaka 18. Nilikuwa raisi mdogo zaidi niliyechaguliwa kuongoza Taasisi ya Bima ya Bulawayo (IIB) nilipoanza kuongoza nikiwa na umri wa miaka 25 tu mwaka 1999 hadi 2000. Majukumu mengine ya kiuongozi niliyobahatika kushika ni pamoja na uenyekiti wa Aids Business Coalition Tanzania (ABCT); mjumbe wa baraza la uongozi wa Muungano wa Wenye Viwanda Tanzania (CTI); mjumbe wa CEO Roundtable Tanzania; na mjumbe wa Chama cha Maraisi Vijana (YPO). Niliwahi pia kuwa mwenyekiti wa Mkutano wa Mwaka wa Siku ya Bima (AIDC) miaka ya 2006 na 2010 na pia kama mjumbe muhimu wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 38 wa Shirika la Bima la Afrika  (AIO) uliofanywa mwaka 2009.

Uongozi wangu hai kazini na katika jamii unajumuisha mikutano rasmi, mijadala na vikao vya mipango juu ya maendeleo ya kiuchumi, kibiashara, kisiasa na kijamii pamoja na marais, mawaziri wa serikali, wafanya biashara, mameya na madiwani kutoka Tanzania, Zimbabwe, Rwanda, Msumbiji, Korea ya Kusini, Uingereza, Kanada na Denmaki.

Baada ya kupata bahati ya kujua mambo mbalimbali na fursa ya kuongoza, ninajisikia ulazima wa kushirikishana maarifa na uzoefu nilioupata na watu wengine pamoja na mashirika mengine. Ninaamini kwamba sisi sote ni viongozi, na kilichobaki tunahitaji kufanya maamuzi ya kukua katika eneo husika.

Mfanyabiashara Mwandamizi

Mimi ni Mbunifu na mpenda matokeo mwenye ujuzi na uwezo uliothibitika kufikia na kupita malengo kwa nia ya ukuaji na maendeleo. Nimejikita zaidi kwenye maendeleo ya makampuni na watu, nikikazania maendeleo ya watu mmoja mmoja na mafanikio na faida ya mashirika. Ninafahamika kwa kuchagua mkakati sahihi wa soko, kuandaa dira na kushawishi ufikiwaji wa malengo husika; muumini imara wa ubepari wenye dhamira njema na watu.

Nimefanya kazi katika maeneo ya huduma za kifedha, hasa bima na huduma ya usimamizi wa majanga kwa miaka 20 iliyopita. Mimi ni Mshauri wa Kujitegemea na ninafanya kazi kama Mwenyekiti wa Kampuni (Binafsi) ya Amua, kampuni inayojishuhulisha na maendeleo ya Uongozi na uwekezaji Afrika, hasa katika nchi za Zimbabwe na Tanzania Kabla ya kazi hii nilihudumu kama Mtendaji Mwandamizi wa kampuni ya African Life Assurance (Tanzania, kampuni ya bima ya muda mrefu ambayo nimeiongoza vizuri hadi kuwa kubwa kuliko zote kwa ukubwa na faida, ikiongezeka kutoka asilimia 10 mpaka kufikia asilimia 47 ya mgawanyo wa soko. Nimefanyakazi pia kama meneja mkuu na afisa mkuu wa Shirika la Liaison Insurance na pia kama meneja mufilisi wa shirika la Aon Risk Services (Zimbabwe). Wigo wa uzoefu wangu unajumuisha soko la majengo na ajali, pamoja na bima ya afya. Nimefanya kazi pia kama afisa mkuu kama mchukuzi wa bima na pia mufilisi wa bima.

Nimehudumu pia katika bodi nyingi za wakurugenzi kama vile za Tanzania Reinsurance Corporation (TANRE), African Life Assurance, Aids Business Coalition Tanzania (ABCT), na East Africa Speakers Bureau (EASB).
Nina diploma ya bima ya Chuo cha Kodi (CII) cha Uingerezana pia cheti cha ‘Mdhibiti Mshiriki wa Majanga’na‘Msimamizi Mshiriki wa Sheria na Utii’kutoka Taasisi ya Bima ya Marekani na Chuo cha Bima za Majengo na  Ajali cha Marekani).

Jitihada za Ujasiriamali-Jamii

Mimi ni muasisi wa falsafa ya Ibariki Afrika na Ubuntu. Hii ni mifungamano ya kijamii inayohusiana na maendeleo ya jamii na uboreshaji wa maisha ya binadamu.

 • Amua Afrika - Amua Africani wakala tendaji yenye kujishuhulisha na ukuzaji wa ubunifu na uwekezaji Afrika. Kwa sasa Amua Africa inasimamia mikataba ya makampuni, huduma na bidhaa mbalimbali kama vile LIMRA, McNulty Re, SMI, pamoja bidhaa mbalimbali za kifedha na kihuduma. Huduma zinazotolewa ni pamoja na ushauri wa kiuongozi, pamoja na uwezeshaji wa kiushikiano na manunuzi (M&A).

 • Ibariki Afrika - Ibariki Africa ni muungano, ambao kwa njia ya vyombo vya habari vya kijamii na kwa njia ya mshikamano wa kijamii, unaojishuhulisha na ukuzaji wa mshikamao na maendeleo ya jamii katika ngazi zote za jamii kuanzia wanajumuiya mmoja mmoja, familia, mitaa, sehemu za kazi, mashirika ya kidini, biashara na serikali.

 • Falsafa ya Ubuntu - Falsafa ya Ubuntu ni mtandao wa kijamii unaokuza maarifa na uelewa wa mifumo maadili na miiko ya Kiafrika inayosisitiza ustawi wa jamii yote kwa ujumla. Maadili haya yanahitajika sana katika jamii ya sasa, ambayo kwa kiasi kikubwa imekuwa na ubinafsi wa kutisha na inayothamini mali zaidi badala ya ustawi wa wengi.

MzungmzajiI Mshawishi

Siku za nyuma mimealikwa ili kuongea kweye taasisi mbalimbali na katika matukio mbalimbali yaliyohusu biashara na uongozi. Baadhi ya taasisi hizo ni:

 • Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) – Shule Kuu ya Uandishi wa Habari
 • Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM)
 • Taasisi ya Wazungumzaji ya Afrika Mashariki (EASB)
 • The Leadership and Lifestyle Forum (LLF)
 • Chuo cha Bima cha Tanzania (IIT)
 • Chuo cha Bima cha Bulawayo (IIB)
 • Mkutano Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Afrika

Baadhi ya mada nilizoongelea katika matukio hayo ni pamoja na:

 • Namna ya kugundua makusudio binafsi kwenye maisha
 • Nafasi ya ubunifu  katika huduma za kifedha
 • Uchaguzi wa kazi kwa vijana
 • Namna ya kuwa kiongozi mzuri
 • Namna ya kuwa meneja mzuri
 • Mbinu za kukufanya uwe WEWE
 • Huduma na Uongozi
 • Malengo katika Maisha yako, Kazi yako na Biashara yako
 • Namna ya kutumia vipaji vyako
 • Namna ya Kuyandisha mawazo kwamishi

Nimetokea kwenye makal na vipindi kadhaa vya runinga  nikiwa ninahojiwa na makala kuhusu umuhimu wa maadili na uaminifu, mapinduzi ya kiuongozi nay a kijamii, ubunifu na mitindo mamboleo. Machapisho na vipindi hivyo ni pamoja na magazeti ya The Guardian, The Citizen, The Chronicle, Daily News, The Business Times, Mint Monday, na vituo vya runinga vya ITV, Channel 10, na EATV.

Kuwawezesha Vijana

Kwa muda wa miaka 22 iliyopita nilipokuwa kijana, nimefanya kazi kuwavutia moyo na kuwavutia vijana. Baadhi ya jitihada kubwa ni pamoja na:

 • Mwanharakati wa Vijana - Nilikuwa mwenyekiti na niliandaa jitihada mbalimbali chini ya Halmashauri ya Vijana ya Jiji la Bulawayo (BJCC) nilipokuwa nikifanyakazi kama diwani na naibu meya mtoto kati ya mwaka 1991 na 1992. Miongoni mwa kazi nilizofanya ni pamoja na Kampeni Dhidi ya UKIMWI na MADAWA YA KULEVYA kwa lengo la kujenga uelewa wa vijana kuhusu madhara ya UKIMWI na VIRUSI VYA UKIMWI. Nilikuwa ni mjumbe muhimu wa kamati ya maandalizi ya Zawadi ya Mwaka ya Mwanamichezo Kijana wa mwaka 1999 nchini Zimbabwe. Nilihudumu pia kamabalozi kijana huko British Columbia, Kanada na kwenye Maigizo ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa mwaka 1991. Mambo mengine niliyofanya ni pamoja na kuchangisha fedha kwa ajili ya watoto maskini na wenye mazingira magumu katika jamii ya watu wa Bulawayo.

 • Mwalimu wa Kujitolea wa Masomo ya Biashara - Nilihudumu kama mwalimu wa kujitolea wa masomo ya biashara katika shule ya sekondari ya Ntabazinduna High School na Chuo cha Wasichana mjini Bulawayo, Zimbabwe kati ya miaka ya 1992 na 1994. Nilifanya haya nikiwa na ajira kamili kama mfilisi kwenye kampuni ya Minet Insurance Brokers.

 • Muwezeshaji wa Biasharana Mfanyakazi wa Kujitolea katika program ya Kampuni ya Junior Achievement - Nilihudumu kama mwezeshaji wa biashara kwenye program ya Kampuni ya  JA Company kwenye shule za sekondari jijini Bulawayo, Zimbabwe kati ya miaka ya 2000 na 2002.  Junior Achievement hufanyakazi kwa kupitia taasisi za elimu na wafanyabiashara kwa nia ya kuwapatia vijana elimu kwa njia ya vitendo katika fani za uchumi na ujasiriamali. Niliwashauri na kuwasimamia wastani wa vijana 30 wa kidato cha nne hadi cha sita katika muda wao wa program ya Kampuni ya JA. Nilikuwa na mikutano hadi miwili kwa wiki kwa kipindi cha wiki 16, niliwasiadia na kuwaongoza vijana kuanzisha na kuendesha biashara ndogo ndogo. Wakiwa chini ya program ya Kampuni ya JA washiriki waliweza kufanya utafiti wa soko, wakachagua aina ya huduma au bidhaa, waliomba na kuchagua kazi, walitengeneza michanganuo ya biashara, waliuza hisa ili kupata mitaji, walizalisha bidhaa na kuziuza pamoja na huduma, walitunza kumbukumbu za biashara, walifanya mikutano na wanahisa, na hatimaye walifunga biashara na kurudisha faida. Haya yalifanyika nikiwa ninafanya kazi kama meneja mfilisi wa kampuni ya Aon Risk Solutions (Zimbabwe).

 • Mzungumzaji na Mshauri Vyuo Vikuu - Nimetoa mihadhara na bado ninaendelea kutoa mihadhara katika taasisi kadhaa za elimu ya juu Dar es Salaam , nikiongelea mada kama vile uchaguzi wa kazi, kufanikiwa, kuwa na malengo katika maisha pamoja na kupanga mipango na dira. Nimeongea Shule Kuu ya Uandishi wa Habari ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), na Chuo cha elimu ya Biashara (CBE).

 • Ibariki Afrika - Nimeanzisha mtandao kuwahamasisha vijana wa Afrika ili wawe chachu ya mabadiliko ambayo wangependa kuyaona duniani kwa njia za Kutafakari, Kushirikiana, Kuungana, Ubunifu, na Kusheherekea.

Kazi za Ushauri

Ninatoa huduma za ushauri katika fani za mikakati ya biashara, na maendeleo ya mitaji ya mashirika na ya watu. Mimi ni Mbunifu na mpenda matokeo na ninaujuzi na uwezo uliothibitika wa kufikia na kupita malengo kwa ukuaji na maendeleo. Nimejikita zaidi kwenye maendeleo ya makampuni na ya watu, nikikuza makuzi ya watu mmoja mmoja kwa lengo la kukuza mafanikio na faida za mashirika. Ninafahamika kwa kuchagua mkakati sahihi soko, kuandaa dira na kushawishi ufikiwaji wa malengo husika; muumini imara wa ubepari wenye dhamira njema na watu.

Nimehusika katika kupanga mikakati ya biashara, kushawishi watu na kutoa mafunzo kwa vikundi na watu mmoja mmoja katika kipindi chote nilichofanya kazi, tangu mwaka 1992. Ingawaje utaalamu wangu ni katika fani ya huduma za kifedha, hususan katika masuala ya bima na udhibiti ya majanga, upenzi na umahiri wangu ni katika eneo la uongozi. Ninaongoza kwa mchakato shirikishi na kuthamini masuala ya maadili, mawasiliano na utamaduni kwa namna ya pekee.Ushiriki wangu mkubwa kwenye jamii umejengwa zaidi kwenye msingi na imani yangu ya dhati kwamba sisi sote ni viongozi. Msingi huu ukijumuishwa na mafanikio yangu katika masuala ya mashirika, uwezeshaji na utoaji katika mashirika ya aina mbalimbali, pamoja na kazi zangu za kujitolea, vinatoa msingi imara ambao kwao ninaweza kuongoza mashirika, vikundi na watu mmoja mmoja hadi kufikia mafanikio.

Ninachanganya utamaduni wa kujali pamoja na tazamo wangu thabiti wa kuona matokeo. Ninatoa mafunzo juu ya namna ya kuwa kiongozi mwenye ufanisi pamoja na namna ya kutambua malengo binafsi ya maisha. Wateja wangu ni pamoja mabenki, mashirika ya bima na sekta za mawasiliano.

Mwandishi

Huwa ninaandika, mahsusi kwa nia ya kujieleza, kuelezea mawazo yangu, maoni yangu, pamoja na ubunifu wangu. Kwa njia ya kujieleza kiubunifu ninataka kuwa Baraka kwa wengine na pia kutumia uwezo wangu wa kuwa mtu mbunifu. Ninaandika juu ya mambo mbalimbali kuanzia namna bora ya kufanya biashara, tafakuri za maisha na pia ushairi.

Burudani

Niliibua kipaji change kimoja kilichojificha jukwaani, na kuweza kupata ziada ya dola 10,000 kwa ajili ya hisani.  Kwa njia ya maigizo ya kusimama katika Maonyesho ya Vichekesho ya Vodacom, niligawana jukwaa na mchekeshaji maarufu wa runinga Barry Hilton wa Afrika Kusini anayefahamika duniani kote. Nikifurahia upande wa vichekesho,nilialikwa pia kuchekesha kama tukio la ufunguzi wakati wa onyesho la saksafoni la muziki wa jazi wa Bobby Rickets.Nilijaribu pia kushiriki kwenye igizo la Moment of Truth, nikiigiza katika nafasi ya mpelelezi mkatili wa siri. Zaidi ya hayo, nimefanya kazi kama mshereheshaji katika matukio makubwa ya mashirika na matukio mengine ya hisani.

Nilibuni vazi ambalo lilitokea kwenye tangazo biashara la TV kwa niaba ya duka moja maarufu la rejareja la Power Sales, kampuni tanzu ya Pepcor SA.

Safari

Nilipokuwa mtoto mdogo safari yangu muhimu ilikuwa ni kupanda basi kutoka Zimbabwe vijijini kuelekea jijini. Nilipenda sana kusafiri, na hata leo bado ninapenda kusafiri na kufahamiana na watu mbalimbali na pia tamaduni mbalimbali. Nimebarikiwa kutembelea nchi zisizopungua 30 katika mabara ya Afrika, Ulaya, Asia, Mashariki ya Kati na Marekani ya Kaskazini. Kufahamu tamaduni na lugha za watu wengine husaidia kuleta maelewano. Pia upenzi wangu wa safari unachangiwa na upenzi wangu wa historia. Kusafiri huniwezesha kutembelea maeneo muhimu ya kihistoria, maeneo ambamo maamuzi makubwa yalifanywa na matukio makubwa yalitokea. Maeneo hayo ni pamoja na Zimbabwe Kuu, mahali ambapo ndipo yalikuwepo makao makuu ya Ufalme wa Mwenemutapa (ukifahamika pia kama Ufalme wa Monomotapa)kwa karne nyingi, Roma, Paris, Berlin, Dakar, Bagamoyo na Zanzibar, sehemu ambapo biashara ya watumwa ilifanyika kwa kiasi kikubwa.

Tunzo & Kutambulika

Kati ya tunzo nyingi nilizowahi kupata zimo hizi zifuatazo:

 • Uanachama wa Jukwaa la Crans Montana Forum of New Leaders for Tomorrow - 2013
 • Mwanachama wa Ushirika wa Uongozi wa Askofu Mkuu wa Tutu unaofadhiliwa na Taasisi ya Afrika ya Uongozi (AfLI) na Chuo Kikuu cha Oxford - 2011
 • Tunzo ya Bodi ya Wakurugenzi ya African Life Assurancekwa Uongozi Uliotukuka - 2011
 • Iliyofanya vizuri zaidi barani Afrika mwezi Juni 2008
 • Tunzo ya Utumishi Uliotukuka wa Junior Achievement Zimbabwe “kwa ajili ya Huduma Iliyojipambanua kwa Vijana na Jamii - 2002