Jinsi ya Kuleta Mabadiliko Duniani

Subscribe the RSS Feed

Subscribe to Syndicate
9 August 2013 - 12:00am -- charles

(Mabadiliko madogo yanaweza kuleta matokeo makubwa!)

Nilipokuwa mdogo mara nyingi nilikuwa nikihuzunishwa na matatizo yaliyokuwa yanaikabili jamii, na nilijiuliza ni sababu gani zilisababisha watu wateseke kwa umaskini, maradhi na mateso mengine. Kasha niliwaza ni kwa namna gani hali hii inaweza kuboreshwa; nilwaza juu ya ufumbuzi wa kuwasaidia watu maskini au namna ya kuleta aamani ambayo imejaa haipo katika dunia hii, lakini pia nikawaza, “Mimi ni nani wa kudhani kwamba ninaweza kuibadili dunia?”

Kwa kadiri nilivyoendelea kukua na kupata ujasiri nikatambua kwamba kwa hakika ninaweza kuwa na mchango na kuleta mabadiliko – nyumbani, shuleni na baadae kazini na kwenye jamii kwa njia ya mawazo yangu, kufanya kazi kwa jitihada zaidi, kujitolea, na kuwasaidia wenye shida.

Ifuatayo ni miongozo ya namna unavyoweza kuchangia mabadiliko duniani, iwe ni kazini kwako, kwenye jamii au nyumbani:

  1. Ongeza Thamani – Njia bora zaidi ya kuchangia mabadiliko duniani ni kwa njia tu ya kujifunza kuongeza thamani kwenye mazingira na maisha yako. Kuongeza thamani kuna maana ya kufanya hali kuwa bora zaidi ya ilivyokuwa. Inaboresha kwenye huduma, bidhaa, mahusiano, na kwa jamii nzima. Unapotambua ulazima wa mabadiliko na kujifunza namna ya kuboresha unajipambanua katika yale unayoyafanya. Hii hukuwezesha kuyafanya maisha yako kuwa bora zaidi, huduma kuwa nzuri na za kuaminika zaidi, na pia kufanya bidhaa kuwa na bei ndogo zaidi na zenye kuleta faida zaidi.
  1. Ubunifu – Fikiria kwa namna pana zaidi na thubutu kuwa tofauti na wengine. Ujasiri huu utakuwezesha kuwa mbunifu. Ubunifu unatuwezesha kutatua matatizo.
  1. Vipaji na Karama – Vifahamu na vitumie vipaji na uwezo wako kwa kadiri uwezavyo. Hukupewa vipaji hivi kwa manufaa yako tu lakini zaidi kwa kuinufaisha jamii. Wale ambao hutumia vipaji vyao kwa uaminifu na kwa jitihada, na wanafanya hivyo kwa manufaa ya kuboresha maisha kwa ajili yao na kwa ajili ya wengine wanauhakika wa kufanikiwa katika yote wayafanyayo.
  1. Shiriki – Ni mihimu kushirikiana na watu wenye mawazo kama ya kwako na ambao wanapendelea mambo kama ya unayoyapenda wewe, na ambao wana tamaa ya kuleta mabadiliko juu ya hali hizo. Kushirikiana na watu wengine huleta mawazo mengi na namna tofauti za kufanya mambo, pamoja na kufahamiana na watu wengine, mambo ambayo huongeza mafanikio katika jitihada zako.
  1. Panga –Nia yoyote ya kubadili hali fulani inahitaji kuchukua hatua, na kila hatua hainabudi kupangwa na kuwezeshwa ili ifanikiwe. Tafakari shuhuli zote zinazohitajika katika kukuwezesha  kufikia lengo lako. Ili uweze kupanga unahitaji kuelewa unataka mabadiliko gani pamoja na matokeo yake. Katika chaguo la kupanga unapata fursa ya kutathmini fursa mbalimbali na kuchagua moja ambayo ni bora zaidi. Simamia na tathmini maendeleo ya jitihada zako ukilinganisha na mpango-mswaada wako.

Kwa bahati mbaya, watu wengi hukubali na kupokea vitu kama vilivyo, hata kama vitu hivyo huwasababishia mateso wao wenyewe na wengine. Matokeo yake no kwamba hawatafuti njia mbadala za mabadiliko na maboresho. Hii ni kwa sababu ama ya wao kutojua cha kufanya au wanategemea mtu mwingine kama serikali au mwajiri au majirani washuhulikie hali ambayo inahitaji kubadilishwa. Ninakuhamasisha ufanye jitihada ufanye kila unachoweza ili kuleta mabadiliko.