Faida na Tuzo za Uongozi wenye Mafanikio!

Subscribe the RSS Feed

Subscribe to Syndicate
5 August 2013 - 9:35pm -- charles

Kama viongozi wa mashirika, mameneja huchagua shuhuli, mikakati, na mbinu ambazi zitztumiwa na timu katika kutimiza vipaumbele na malengo. Ili kuweza kutimiza hayo wanazo raslimali mbalimbali za kufanikisha hayo, ikiwa ni pamoja na nguvu na hamasa  ya idara au mashirika yao, ubunifu na mawazo, uwezo wa kufanya kazi na rasilimali fedha zilizopo. Kuna faida  na tuzo mbalimbali kwa uongozi bora, na zinajumuisha zifuatazo:

  1. Fedha: Nyongeza ya kipato na motisha huwawezesha mameneja kufurahia maisha mazuri, wakitunza familia zao vizuri na pia wakifanya maandalizi mazuri kwa maisha yao ya baadae. Kipato kikubwa humuwezesha pia meneja kuwasaidia wengine wasio na kipato cha kutosha.
  1. Kuridhika: Hali ya kujisikia kuridhika na utekelezaji wa mipango yako, kuzishinda changamoto, na kutumia fursa katika kutimiza malengo binafsi nay ale ya timu. Hili ni jambo la kujivunia.
  1. Mafanikio ya Shirika:  Unapata hisia ya thamani na maana katika kutoa huduma na bidhaa zilizo na maana kwa wateja. Ukuaji wa shirika ni lazima utafsirike kwa ongezeko la watu  wanaoijenga biashara, pamoja na ukuaji na uwezekano wa matumizi ya raslimali mpya. Huu ni mchango mkubwa na ni muhimu kwa uchumi wa jamii pamoja na wa taifa.
  1. Mvuto:  Mafanikio ya meneja na ya timu ni mfano mvuto kwa wengine ili wawe waadilifu, wabunifu, wawe na maono makubwa pamoja kutamani mambo makubwa.  Jambo hili ni muhimu zaidi kwa vijana, hasa kwa sababu wao ni tegemeo la taifa la kesho.
  1. Mapatano ya Kudumu: Meneja anapoajiri watu kwa kufuata utaratibu na weledi hutoa fursa ya kuunda mtandao mahusiano ya kudumu na marafiki, washirika na wateja.
  1. Umaarufu: Uongozi bora humpa meneja sifa nzuri miongoni mwa wenzake na jamii. Umaarufu huu hutokana na ukweli kwamba watu hupokea, hukubali, na huheshimu mtazamo, mafanikio na mchango wa meneja kwa mafanikio ya jamaa zao, na maendeleo ya sehemu yao ya kazi, pamoja na yale ya jamii. Umaarufu huwa ni matokeo ya uongozi bora. Kamwe umaarufu usikuliwe kuwa kigezo cha kumfanya mtu atafute nafasi ya uongozi.

Sote tuna uwezo wa kuwa mameneja, na si hivyo bali mameneja wenye mafanikio. Safari ya kuwa kiongozi bora huanza na kujiongoza wenyewe vizuri kila siku katika kila jambo ulifanyalo, katika maisha binafsi na yale ya weledi. Uongozi hautokani na cheo cha mtu, na kwa sababu hiyo hauwahusu tu wale ambao wapo tayari katika nafasi za uongozi. Kwahiyo songa mbele na uwe meneja bora kwa kadiri uwezavyo na furahia maslahi mengi yanayoambatana na kuwa meneja mzuri!