Charles WashomaMwafrika Halisi & Raia wa Dunia

Nilipokuwa mdogo, nilipata mtazamo hasi (hatarishi, usiojenga, wenye kukatisha tamaa) wa kitamaduni, na matokeo yake nilijenga mtazamo (hasi) na nikadharau urithi wangu wa Kiafrika. Hatimaye nikagundua kwamba hakuna utamaduni wowote ule ulio kamilifu, kwahiyo nikaamua kuchagua mambo mazuri yaliyomo kwenye tamaduni zote. Pamoja na shauku yangu ya kuipenda dunia nzima, hii ni moja ya sababu zinazonifanya nipende kusafiri na kuchanganyika na watu  duniani kote. Polepole na kadri nilivyozidi kuongezeka umri, nikaanza kuuthamini urithi wangu kwa nguvu na kwa ari zaidi.

“Siku zote nimefurahaia kuwepo Afika na kuwa Mwafrika.Ninathamini na kuheshimu urithi wangu wa Ubuntu, Utu, naHunhu, unaojumuisha hisia nzito ya ubinadamu. Ninatambua pia nafasi maalumu na wajibu tulionao wote kama raia wa dunia.”

Biography

Nina upenzi zaidi na falsafa ya Kiafrika ya Ubuntu, inayokazia umuhimu wa ubinadamu na ustawi wa jumuiya. Utamaduni huu umeenea kwenya jamii zote za Kiafrika. Kwa mfano, katika lugha ya Kishona falsafa ya ubuntu inafahamika kama Hunhu na kwa Kiswahili inafahamika kama Utu.

Pia ninajivunia kuwa raia wa dunia kwa sababu ninatambua kwamba sisi ni wa mbari moja ya binadamu. Mustakabali na ustawi wetu kama binadamu unategemeana. Kwa miaka mingi nimejihusisha katika shuhuli mbalimbali zenye lengo la ukuzajia uelewa juu ya dhana ya Ubuntu, na kwa kufanya hivyo kuongeza uwezo wa kiuongozi, amani na uelewa. Mimi ni muasisi wa www.UbuntuPhilosophy.Org.in kwa nia ya kushawishi ufahamu wa falsafa ya Ubuntu na umuhimu wa jumuiya kwa lengo la kusaidia kujenga na kubadili jumuiya Afrika nzima na duniani kote.

Bookmark and Share

Naamini kwamba kila mtu anaweza kufanya vizuri hapa duniani kwakuishi kwa malengo maalumu; hii ni pamoja na kutumia vipaji vyako, kujua sababu za kuwepo kwako hapa duniani, kutekeleza dira pamoja na kufanyia kazi vipaji vyako.

Dhima

Lengo na dhamira yangu ni kuwa mtumishi wa ujumbe wa matumiani unaotia moyo wote ili kutuwezesha kujenga jamii shirikishi zenye madhumuni ya tija za kimaendeleo. Mtizamo wangu ni kutumia na rasilimali nilizo nazo katika kufanikisha azma hii.

Dira

Dira yangu inahusu Afrika na ulimwnegu mzima ambayo ninaitakia mustakabali wenye mvuto zaidi. Mustakabali ninao uona ni ule wa kuona kuwa Waafrika wameungana na wanafanya kazi lengo moja la kujenga umoja na mshikamano. Ninaamini kuwa sisi kama Waafrika. Tunahitaji uelewa mkubwa zaidi katika jamii yetu ili tu weze kuungana tu songe mbele ili tushike nafasi yetu stahiki hapa duniani kama washirika tu ki elekea kwenye mustakabali ulio boka na wenye matumaini zaidi.

Maadili

Uongozi unaanza kwa mtu binafsi na hivyo ni muhimu kuwa na maadili mema utakayotumia kuongoza maneno na matendo yako ya kila siku.

Maadili yangu yamejengeka kwenye nguzo kuu tatu muhimu:

 1. Mungu: Ni imani yangu ya msingi kuwa Mwenyezi Mungu ndiye muumbaji asilia. Ufahamu wangu na uabudu wangu umejengeka kwa msingi wa injili ya Bwana wa milele aliyefufuka, Yesu Kristo.
 2. Urithi wa Kiafrika: Ninathamini na kuheshimu urithi wangu wa Ubuntu, Utu, Hunhu!, ambao unajumuisha hisia za ubinadamu.
 3. Maadili ya Kishujaa: Nidhamu, heshima, na ujasiri ni mambo ya msingi yanayaoongoza yote ninayay.

 

Ujumbe kwa vijana

Kigezo muhimu kwenye maisha ni namna unavyotafsiri na kukabiliana na hali na mazingira mbalimbali. Ni muhimu kuwa na mtazamo chanya juu ya maisha yako mwenyewe na dunia kwa ujumla. Ninapenda kukushirikisha kanuni kumi za zinazoweza kusaidia kutimiza lengo hilo:

 • Ujue sababu za uwepo wako duniani, na ishi maisha yenye dira ili uweze kutimiza malengo makubwa ya kukuzidi wewe mwenyewe.
 • Usiruhusu mazingira yako binafsi kuwa kikwazo kwako.
 • Ni muhimu kwenye maisha kufanya maamuzi na kuyatekeleza kwa dhati.
 • Haijalishi kwamba umefanya maamuzi sahihi au la, muhimu zaidi ni kwa namna gani unayatekeleza vizuri maamuzi uliyoyafanya.
 • Mara zote timiza yale unayoahidi na uheshimu namna watu wanavyokuthamini.
 • Ukubali pale unapofanya makosa na jifunze kwa kila hali.
 • Ingawaje pesa ni muhimu usithamini mali kupindukia.
 • Epuka ulevi, madawa ya kulevya, na ufedhuli, kwa sababu mambo kama hayo yana madhara kwa mtu yeyote yule.
 • Jitahidi kuhusiana na watu ambao watakuwa na athari chanya kwenye maisha yako, na wewe mwenyewe uwe na athari chanya kwa wengine.
 • Usiigize na kujifanyisha tofauti na ulivyo lakini kila mara jitahidi uwe ulivyo.